Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

WAFANYAKAZI WANAWAKE WA TRC WASHIRIKI SIKU YA WANAWAKE DUNIANI


news title here
09
March
2021

Wafanyakazi Wanawake wa Shirika La Reli Tanzania washiriki siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa kimataifa kila mwaka Machi 08.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kitaifa yamefanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Mlimani City ambapo Mgeni Rasmi akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan huku kauli mbiu ikiwa “Wanawake katika Uongozi, chachu kufikia Dunia yenye Usawa”

Judith George, Mfanyakazi wa Shirika la Reli katika Idara ya Uhasibu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wanawake TRC ameeleza kuwa “Wanawake wa TRC ni miongoni mwa wanawake ambao tunashiriki kila mwaka siku hii, tunamshukuru sana Mkurugenzi Mkuu Ndugu Masanja Kadogosa anatuwezesha kukakimilisha shughuli hii tunamuombea aendelee hivi kila mwaka”

Pia Wanawake wafanyakazi wa TRC wametoa rai kwa wanawake wengine kuchangamkia fursa zilizopo katika mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR ili kujikwamua kiuchumi, wameongeza kuwa Shirika linawakaribisha wanawake kutembelea Mradi huo kwani limeweka utaratibu mzuri wa kupata taarifa za mradi huo ikiwemo namna ya kushiriki fursa zilizopo.

Aidha, wanawake hao wamefurahi kushiriki maadhimisho hayo na wanafarijika kwa kuwa kauli mbiu ya mwaka 2021 inaakisi kwa vitendo ushiriki wa wanawake katika uongozi ndani ya Shirika la Reli na wamepongeza wanawake wote waliopo katika uongozi ndani ya Shirika kwa utendaji wao mahiri.