Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

WAFANYABIASHARA, VIJANA PAMOJA NA VIONGOZI WA SERIKALI WA VIJIJI WAJIVUNIA MRADI WA UBORESHAJI WA RELI YA KATI


news title here
15
July
2020

Shirika la Reli Tanzania limefanya kampeni ya ushirikishwaji wa jamii katika maendeleo ya mradi wa uboreshaji wa reli ya kati kuanzia Kilosa hadi Isaka, Julai 2020 hivi karibuni.
Kampeni hiyo iliyofanywa na Maafisa mbalimbali kutoka TRC pamoja na maafisa kutoka Kampuni ya mkandarasi CCECC wamehakikisha kila jamii inapata fursa ya kufahamu mambo ya msingi kabla mradi huo wa uboreshaji wa reli ya kati kufikia ukingoni Julai 30 mwaka huu.
Hata hivyo wafanyabiashara, vijana pamoja na viongozi wa vijiji tofauti wameishukuru sana Serikali pamoja na TRC kwa kuleta mradi huo kwani umeleta manufaa makubwa kwenye maeneo yao.
Manufaa hayo ni pamoja na ukuaji wa biashara kama vile mama ntilie, watu wa masoko, maduka pamoja na ongezeko la kipato kwa wanajamii kwa kufanya biashara kwa wingi katika maeneo yote ambayo yamepitiwa na mradi.
Pia Vijana wengi wamepata fursa ya kupata ajira katika mradi zikiwemo za uondoaji wa reli ya zamani na utandikaji wa reli mpya na nyanja tofauti ambazo wamepatiwa katika uboreshaji wa mradi huo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Karangasi Pascal Mungo ametoa shukrani za dhati kwa Serikali ya awamu ya tano na kusema kuwa mradi huo umewakwamua vijana wengi ambao hapo awali walikua wakizagaa mtaani na kufanya vitendo vya kihalifu.
“Kwa sasa vijana wameacha vitendo vya uhalifu baada ya kupata ajira kwenye mradi na wanaendelea kuchapa kazi" alisema Bw. Mungo.
Vilevile Mradi huo umeleta manufaa katika baadhi ya vijiji kwa kuchangia maendeleo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa kwa kutoa mifuko ya saruji pamoja na upakaji wa rangi wa madarasa, ujenzi wa matundu ya vyoo mashuleni, ujenzi wa kisima cha maji, ukarabati wa barabara, na pia utoaji wa madaftari mashuleni.