Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​WADAU WA USAFIRISHAJI NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI WATEMBELEA MDARI WA SGR


news title here
02
April
2022

Wadau wa usafirishaji nchi za Afrika kutoka katika taasisi ya Ushoroba wa Kati wametembelea mradi wa reli ya kisasa - SGR kipande cha kwanza kuanzia katika jengo la stesheni ya Dar es Salaam hadi kilometa nne Machi , 2022.

Kaimu Mkurugenzi wa miundombinu ya reli Mhandisi Faustin Kataraia amesema kuwa taasisi hiyo inahusika na kuanzisha mawazo ya miradi mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki ambayo baadae inatafutiwa ufadhili ama ujenzi na kuanza kujengwa.

“Wamekuja kwa lengo la kuangaalia maendeleo ya mradi huu wa SGR ili kuzidi kupata mawazo tofauti na mapya” alisema Mhandisi Kataraia.

Mhandisi Kataraia ameeleza kuwa kazi za msingi ujenzi wa SGR zimekamilika ikiwemo kuweka tuta, kuunganisha reli pamoja na nyaya za umeme kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, na Morogoro hadi Kilosa.

“Sasa hivi hatua tuliyopo tunajaribu mtambo mmoja baada ya mwengine kabla hatujaingiza umeme” alisema Mhandisi Kataraia.

Naye Katibu mtendaji wa Ushoroba wa Kati Bw. Dukundane Dieudonni amesema kuwa wadau wameona uthubutu uliofanywa na nchi ya Tanzania kujenga mradi mkubwa wa kimkakati wa reli ya kisasa - SGR.

“Uthubutu huu umewapa hamasa nchi nyingine za ushoroba wa kati, uwekezaji ni mkubwa na umetumia pesa nyingi sana “ alisema Bw. Dukundane.

Aidha, Bw. Dukundane alisema kuwa kupitia mradi huu mafanikio ya kibiashara yatakuwa mengi hasa upande wa mizigo kutokawia kutoka bandari ya Da es Salaam kwenda nchi za jirani za Kongo, Uganda, Burundi, Rwanda.

“Kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi mpakani mwa Kongo ni kilomita 1300 na kasi ya treni hii ya kisasa itarahisisha sana usafiri" alisema Bw. Dukundane.

Vilevile mjumbe wa Bodi wa Chama cha Usafirishaji wa Malori - TATOA Bw. Shakanyi Wagora amesema kuwa mradi wa SGR utaleta tija katika sekta ya usafirishaji Tanzania na kuendelea kushiriki kwa pamoja katika kukuza uchumi wa nchi.