Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

TRENI YA MCHONGOKO YAWAFURAHISHA WABUNGE WA DRC


news title here
07
November
2024

Wabunge wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Congo (DRC) watembelea Shirika la Reli Tanzania (TRC) makao Makuu Jijini Dar es Salaam Novemba 07, 2024.

Lengo la ziara ya wabunge hao ni kujifunza na kujionea maendeleo ya Shirika la Reli Tanzania kupitia ujenzi na uendeshaji wa reli na treni za kiwango cha Kimataifa zinazoendelea kutoa huduma kati ya Dar es Salaam na Dodoma.

Akiongea wakati wa ziara hiyo Mkuu wa msafara wa wabunge hao Mhe. John Banza amesema kuwa ujenzi wa reli ya SGR umedhihirisha uwezo wa serikali ya Tanzania katika kuwatumikia wananchi kwa hali na mali na kuleta maendeleo ya kiuchumi haswa katika sekta ya uchukuzi.

"Tumesafiri jana kutoka Dodoma hadi Dar es Salaam, tumepanda treni ya mwendokasi ya mchongoko, kwa kŵeli tumejifunza mengi na zaidi ni kwamba nchi ya Tanzania inafanya vyovyote kuleta maendeleo, kwa ujenzi wa reli ya SGR ni muujiza wa Afrika" alisema Mhe. Banza.

Aidha, Mhe. Banza ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kalemie, ameongeza kuwa mazungumzo baina ya wabunge wa DRC na Manejimenti ya TRC yamefungua njia na mawazo chanya katika utekelezaji wa ujenzi wa SGR nchini Congo.

"Tumekuja kuona ni namna gani Tanzania wameweza kujenga reli hii ya muujiza Afrika, tumepata mwanga mkubwa namna walivyo tekeleza na sisi Wabunge ni jeshi kubwa tutaenda kuhimiza serikali kuharakisha ujenzi wa SGR" alisema Mhe. Banza.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Senzige Kisenge, amesema kuanza kwa shughuli za uendeshaji wa treni za SGR umezidi kuchochea maendeleo ya nchi pamoja na wananchi kwa ujumla kutokana na uwezo wa treni kubeba watu wengi kwa pamoja na mwendo kasi.

Ujenzi wa reli nchini DRC utachochea ushirikiano kati ya nchi hizi mbili na kukuza diplomasia katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa.