Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

TRC YASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO NA WADAU KATIKA KUBORESHA MAISHA YAJAMII ZINAYOISHI PEMBEZONI MWA RELI


news title here
30
July
2020

Shirika la reli Tanzania – TRC limekutana na kutiliana saini mkataba wa makubaliano na wadau ili kuleta maendeleo katika jamii zinazoishi pembezoni mwa reli na wale ambao ardhi yao imetwaliwa na TRC kwa ajili ya kupisha mradi wa ujenzi wa SGR. Hafla imefanyika katika ukumbi wa TRC makao makuu jijini Dar es Salaam hivi karibuni Julai 29, 2020.

Lengo la hafla hiyo ni kuwakutanisha wadau tofauti ambao wamekuwa karibu na shughuli za utekelezaji wa miradi ya Shirika hususani Mradi wa Ujenzi wa reli ya Kisasa – SGR na Mradi wa Uboreshaji wa Reli ya Kati – TIRP na kujadili namna ya kupunguza athari hasi zinazotokana na miradi ili kuleta maendeleo kwa jamii zilizopo katika maeneo ya miradi.

Hafla hiyo imehudhuriwa na wadau tofauti zikiwemo taasisi za serikali ikiwemo kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam - UDSM, Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi - VETA, Shirika la Maendeleo ya Viwanda vidogo - SIDO,Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF, Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Jeshi la Polisi, Asasi zisizo za Kiserikali (NGO’s), Kampuni ya Korail, Yapi Merkezi na Shirika la Uhandisi na Ujenzi la China – CCECC.

Aidha, mkataba huo pia umesainiwa kwa ajili ya kuendelea kuboresha maisha kwa jamii ambazo zinapatikana pembezoni mwa njia ya reli ambao unalenga kutoa msaada zaidi kwa kaya zilizopitiwa na mradi.

Mipango ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kuboresha jamii ni pamoja na mafunzo ya usimamizi wa fedha kwa kaya zilizopitiwa na mradi, namna ya kupata ardhi na usalama wa umiliki, uboreshaji wa ardhi kwa kuongeza tija ya ardhi na kilimo, uhamaji wa mifugo na upatikanaji wa maji kwa mifugo, Kilimo na matumizi ya kawaida, kuasisi mpango wa uangalizi na usimamizi wa ukatili wa kijinsia pia kufahamiana ili kuendelea kushirikiana katika mamboyatakayojitokeza kwenye miradi.

TRC inatambua mchango mkubwa unaotolewa na taasisi hizi za jamii, hivyoTRC ina kila sababu ya kuongeza nguvu na ushirikiano wa karibu na taasisi hizi ili kuleta matokeo chanya katika utekelezaji wa miradikwa kuwa miradi hii imeletwa ili kuleta faida kwa wananchi na si kuleta madhara.

Katika kuhakikisha malengo haya yanatimia TRC kwa kushirikiana na taasisi za serikali kama TASAF, SIDO, UDSM, VETA na zisizo za serikali(NGOs) zitahakikisha mambo ya kijamii, mazingira na kiuchumi yanakuwa sawa kwa wananchi wote walilengwa kwa mipango hii endelevu.

Wadau wametoa shukurani na pongezi kwa TRC kwa kufungua mkutano huo ambao utakuwa na manufaa makubwa kwa TRC na jamii inazozunguka mradi kupitia ushirikishwaji na makubaliano yaliyotiliwa saini katika mikataba hiyo.

TRC inatarajia ushirikiano mzuri kutokakwa wadau na washiriki katika kutekeleza mipango iliyopendekezwa na kukaribisha mawazo mapya na uzoefu mbalimbalikutoka kwa wadau ili kuendelea kupata uelea wa pamoja na wadau ili kufanikisha utekelezaji wenye tija , ubora na ufanisi mzuri zaidi.