Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

TRC YAENDELEA NA ZOEZI LA ULIPAJI FIDIA ILI KUPISHA UJENZI WA RELI YA KISASA MOROGORO – MATUKUPORA


news title here
15
October
2019

Shirika la Reli Tanzania – TRC laendelea na zoezi la ulipaji wa fidia kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro kwa lengo la kupisha ujenzi wa reli ya kisasa – SGR awamu ya Pili Morogoro – Matukupora, ambapo zoezi limeanza kwa wakazi wa kijiji cha Kimambila, kata ya Lubungo wilayani Mvomero mkoani Morogoro hivi karibuni Oktoba 2019.

Ujenzi wa reli kisasa awamu ya pili Morogoro – Matukupora wenye urefu wa Kilometa 422 unaendelea kwa kasi na umefikia zaidi ya asilimia 17, kazi kubwa ikiwa ni utengenezaji wa tuta la reli, madaraja na vivuko, uchorongaji wa milima kwa ajili ya kujenga mahandaki yatakayopitisha reli ya kisasa ambapo kwa upande mwingine imekuwa kivutio kikubwa. Pia mkandarsi Yapi Merkezi hivi anakaribia kutandika reli katika kipande hiko cha Morogoro – Makutupora.

Jumla ya wananchi 167 wanatarajia kulipwa fidia ya rasilimali zao ambazo Shirika limetwaa kwa ajili ya kupitisha mradi wa SGR, wananchi hao watalipwa fidia ya rasilimali ambazo ni pamoja na ardhi, nyumba, miti na mazao.

Aidha Zoezi limeendeshwa na maafisa kutoka Shirika la Reli Tanzania wakishirikiana na wenyeji wao, Mtendaji wa Kijiji pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji hicho ambapo wametoa shukrani zao na pongezi kwa shirika la reli kwa kutimiza ahadi ya kulipa fidia wa wananchi ambapo itawasaidia wananchi kupisha maeneo hayo kwa wakati na kumfanya mkandarasi kuendelea na mradi.

Kwa upande wake Bi. Beatrice Shayo ambae ni Mtendaji wa Kijiji cha Kimambila amewapongeza maafisa wa Shirika la Reli kwa kuendesha zoezi kwa muda sahihi na kwa ufanisi amani na usalama ikiwepo eneo la tukio, hata hivyo amewaomba wananchi kutumia fedha kwa maendeleo ya familia zao na kijiji kwa ujumla hasa kujenga nyumba bora za kisasa pamoja na kuanzisha biashara ambazo zitainua uchumi wa familia mpaka ngazi ya kijiji.

“Ninawaomba wanakijiji waliolipwa fidia wakazi geuze fedha hizi kuwa chachu ya maendeleo hasa katika kuboresha maisha kwa kujenga nyumba bora na imara lakini pia kuanzisha biashara ambazo zitawaongezea kipato na kukuza uchumi wa familia mpaka uchumi wa kijiji na kuifanya Kimambila kuwa mfano wa kuigwa kwa maendeleo” alisem Bi. Beatrice