Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​TRC YAENDELEA NA ZOEZI LA KUHAMISHA MAKABURI WILAYA YA BAHI MKOA WA DODOMA


news title here
12
September
2019

Shirika la Reli Tanzania - TRC laendelea na zoezi la Kuhamasisha Kuhamisha makaburi katika Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Kwa lengo la kupisha Ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR kipande cha Morogoro - Makutupora, hivi karibuni Septemba 2019.

Zoezi hilo lilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe.Mwanahamis Munkunda Das Ndugu Jeremiah Mapogona na Mkurugenzi wa Wilaya ya Bahi Ndugu Dkt.Fatuma Ramadhan Maganga, Serikali ya Kijiji na Maofisa toka TRC na Mkandarasi Yap Merkezi.

Zoezi linajumuisha jumla ya makaburi 175 yatakayohamishiwa sehemu maalum zilizotengwa na katika vijiji vifuatavyo, Kigwe, Mzogole, Mpinga, Mapinduzi, Bahi Makulu, na Bahi Sokoni.

Akiongea na wananchi wa Wilaya ya Bahi Afisa Miliki toka TRC Bwana Sweetbert Misango alielezea shughuli nzima na utaratibu wa zoezi la kuhamisha Makaburi .

“Kwenye zoezi zima la kuhamisha vitu muhimu ambavyo vimepitiwa na njia ya Reli vinavyozingatiwa ni Makazi na Makaburi“ alisema Bwana Misango.

Aidha Shirika kupitia Maofisa wake liliwaomba wananchi kuwa wavumilivu pindi taratibu za uandaaji wa daftari la kufuta machozi na pindi litakapokamilika wananchi watapatiwa vifuta machozi kwa lengo la kuwafariji“ alisema Bwana Misango toka TRC”

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamis Munkunda alianza kwa kutoa Shukrani kwa Wananchi kwa ushirikiano waliouonesha kwa kushiriki vizuri zoezi la uthamini pia aliendelea kuwasisitiza kutoa ushirikano kwa serikali na kumuunga mkono Mhe. Rais kwenye Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR .

Lengo la kuwasisitiza wananchi hao ni kuhakikisha shughuli za mradi ikiwemo zoezi hili linakwenda kwa urahisi na mradi unamalizika kwa wakati uliopangwa .

“Tusimuangushe Mhe Rais Magufuli kwani anaimani na sisi hivyo anategemea zoezi hili liishe kwa wakati ili kuendeleza jitihada za kujenga Reli ya Mwendokasi “ alisema Bi. Mwanahamis.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya aliomba serikali za vijiji kuandaa maeneo maalum ya kijiji kwa ajili ya kuzikia na kuwaomba wananchi kuzika katika maeneo hayo maana wilaya ya Bahi bado inakua na mji utatanuka.