Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​TRC KUNYAKUA TUZO KWA UBORA WA KUHABARISHA UMMA


news title here
23
September
2024

Shirika la Reli Tanzania - TRC kupitia kitengo cha Habari na Uhusiano kwa Umma imeibuka kidedea kwa kunyakua tuzo katika tuzo za Uandishi Wenye Tija (Stories of Change) za mwaka 2024 zinazotolewa na taasisi ya Jamii Forums na kuwa taasisi ya Serikali inayohabarisha umma kwa usahihi na wakati, Septemba, 2024.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano kwa Umma Bi. Jamila Mbarouk ameeleza kuwa tuzo hizo ni za kipekee kwa kuwa wananchi wameweza kupiga kura na kuichagua TRC kuwa taasisi ya Serikali inayofanya vizuri katika kuhabarisha umma kwa wakati.

“Jukwaa lililoweza kuchagua kazi za TRC ni jukwaa huru, wananchi wameona ufanisi wa kazi za TRC na kushirikiana nao pindi wanapohitaji ufafanuzi wa taarifa” alisema Bi. Jamila.

Bi. Jamila alisema kuwa tuzo hiyo itaendelea kuleta tija kwa Shirika la Reli Tanzania kwakuwa wananchi wanaona kazi nzuri zinazofanywa na TRC na kuwahakikishia kuwa TRC itaendelea kushirikiana na umma katika kuwapa taarifa kwa usahihi na wakati.

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Jamii Forums Bw. Mexence Melo alisema kuwa pasi na kuwa na malalamiko yaliyojitokeza kabla na baada ya uendeshaji wa mradi wa SGR ila TRC imekua ya kipekee kwa kutoa majibu kwa wananchi na kuchukua hatua kwa wakati.

“TRC ni miongoni mwa taasisi za mfano ambao wamekua wakichua hatua pale yanapotokea masuala ambayo wananchi wanahitaji yafanyiwe kazi” alieleza Bw. Melo.

Shirika la Reli Tanzania limepewa dhamana na serikali kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujenga reli yenye kiwango cha kimataifa na hivi sasa TRC imeanza kutoa huduma za reli hiyo kwa kutumia treni za kisasa zenye kutumia nishati ya umeme.