Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

TRC KINARA AFRIKA KWA UJENZI WA RELI YA SGR


news title here
17
June
2025

Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, imelipongeza Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya uchukuzi kwa kusafirisha abiria na mizigo kwa haraka na kwa wingi kupitia miundombinu ya reli zote mbili za SGR na MGR.

Hayo yebanishwa Juni 17, 2025 na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe. George Simbachawene alipolitembelea banda la maonesho la TRC, wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma kuanzia Juni 16 – 23, 2025.

Mhe. Simbachawene amesema, ujenzi wa Reli ya SGR ilikuwa ni maamuzi muhimu ya kimaendeleo na kisera yaliofanywa naSserikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imeliletea Taifa Ushindi Mkubwa barani Afrika na dunia katika mapinduzi ya Kisekta na kuwa sehemu ya mafunzo kwa nchi nyingi barani Afrika.

Aidha, Mhe. Simbachawene amelitaka Shirika la Reli Tanzania kuendelea kuitumia Reli ya MGR kusafirisha abiria na mizigo ili kuongeza ufanisi na kuwahudumia Watanzania wote wa mijini na vijini kwa kuzingatia hali zao za vipato na maeneo ya kijografia.

“Ujenzi wa SGR ni maamuzi muhimu sana ya kisera yaliofanywa na serikali ya Tanzania, itoshe kusema kwamba Tanzania tumepiga hatua katika hili, SGR imekuwa chachu ya usafirishaji na sisi sote hapa tumeshuhudia hilo , naomba nisitize kwamba TRC msiache kutumia Reli ya MGR, Reli hii imekuwa nguzo kubwa tangu enzi za ukoloni, tusiache kwa kuwa tumepata kipya , Ukipata nguo Mpya Usiache ya Zamani , Reli ya Zamani iboreshwe na iendelee kutumika kukidhi mahitaji ya wananchi wote” amesema Simbachawene.

Shirika la Reli Tanzania limeendelea kutoa huduma za Kidigiti ili kuendana na badiliko ya teknolojia na sera ya utumishi wa umma kama inavyosema Kauli Mbiu ya waka 2025 katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma “Himiza matumizi ya Mifumo ya Kidigiti ili Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchangia Uwajibikaji kwa kuwa na mifumo mbalimbali ya kidigiti kama vili Watumishi Portal ( Employee Self Service), Mfumo wa Manunuzi( Nest), Mfumo wa Malipo ( ERMS) na Kadhalika.