TAASISI ZA UCHUKUZI ZA PANDA MITI STESHENI YA SAMIA DODOMA

June
2025
Shirika la Reli Tanzania (TRC), limeungana na taasisi 14 nyingine zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi kupanda miti takribani 50 katika Stesheni Kuu ya Samia Suluhu SGR) Jijini Dodoma, kuadhimisha wiki ya mazingira Duniani inayofanyika kitaifa Jijini humo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete kuanzia 01- 06, 2025.
Zoezi hilo la upandaji miti ni muuendelezo wa utunzaji mazingira katika sekta ya reli ukiendana sambamba na ujenzi wa reli ya SGR ambao umejikita katika matumizi ya nishati ya umeme ambayo inachochoea utunzaji mazingira na kutoruhusu uchafuzi wa hali ya hewa.
Bwana Bahati Shagihilu mwakilishi wa mkurugenzi wa usalama na mazingira wizara ya uchukuzi, akizungumza wakati wa zoezi hilo la upandaji miti, amesema kuwa Wizara ya Uchukuzi pamoja na Taasisi zake zitaendelea kufanya shughuli za kiuchukuzi kwa kuzingatia utunzaji na uboreshaji wa mazingira kwa maendeleo zaidi ya nchi.
Sambamba na hilo Bwana Bahati ametoa wito kwa TRC kuitunza vyema miti iliopandwa ili kuweka mazingira ya stesheni Kuu ya Samia nadhifu na kuongeza mvuto wa kijani.
Shirika la Reli Tanzania limejikita katika utunzaji mazingira kwa kudhibiti matumizi ya plastiki na taka zinginezo zinazozalishwa katika uendeshaji wake hususani treni za SGR na MGR.
Siku ya mazingira duniani huadhimishwa Juni 05 kila mwaka na kwa mwaka 2025, kauli mbiu yake ni Mazingira yetu na Tanzania Ijayo Tuwajibike Sasa,Thibiti Matumizi ya Plastiki.