Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​SHIRIKA LA RELI TANZANIA LAIBUKA KIDEDEA KWA KUPATA TUZO YA KURASA BORA YA SERIKALI MTANDAONI


news title here
17
February
2021

Shirika la Reli Tanzania laibuka kidedea kwa kupata tuzo ya kurasa bora ya serikali mtandaoni iliyopokelewa kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na uongozi waShirika la Reli Tanzania - TRC katika ukumbi wa Akemi Februari 16, 2021.

TRC imeshinda Tuzo hiyo baada ya kushindanishwa katika kipengele cha Kurasa Bora ya Serikali Mtandaoni inayohabarisha wananchi ambapo mashindayo hayo yaliyoandaliwa na kampuni ya Serengeti Bytes kwa kushirikisha mashirika na taasisi zote za serikali.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kungu Kadogosa amesema kuwa tuzo hiyo ni kubwa kwa shirika na inadhihirisha kuwa kinachofanyika katika shirika la reli wananchi wengi wanaona kupitia taarifa zake na kinaleta manufaa na manufaa katika nchi.

“Sisi tumeona ni jambo kubwa na hata katiba yetu ya taifa inatambua vitu vinavyofanyika ndani ya serikali lazima watu wawe na taarifa“ aliongezea kuwa “tunatimiza sUala la kisheria na vilevile tunatendea haki watanzania wajue pesa yao ya kodi inakwenda wapi” alisema Ndugu Kadogosa.

Pia Ndugu Kadogosa alieleza kuwa ushindi huo umeleta matokeo kwa wananchi na kuwa watu zaidi ya milioni saba wanaona na wanahabirika kupitia mtandao wa TRC Reli TV wa Youtube na pia kupitia mitandao mengine na Instagram, Twitter, Facebook na Tovuti ya TRC.

Naye Mkurugenzi Mtendaji katika kampuni ya Serengeti Bite Bw. Michael malya amesema kuwa TRC ilishindana kama kipengele cha serikali mtandaoni na wameibuka kidedea baada ya kupata kura nyingi kutoka kwa wananchi. “TRC ilipigiwa kura kama taasisi bora ya serikali ambayo inafanya matumizi bora ya mtandao ya kijamii katika kufikia umma” alisema Bw. Malya.

Aidha Bw. Malya ameipongeza sana TRC na kusema kuwa TRC imetoa hamasa kwa taasisi nyingine za serikali kujifunza na kuendelea kuboresha kwa kufanya kazi nzuri kupitia majukwaa ya mitandao ambayo wananchi wengi wanaona kazi zinazoendelea kiurahisi zaidi.

“Lengo kuu la Tuzo za kidigitali ni kuongeza ubunifu katika matumizi ya teknolojia hasa za kidigitali na pia kuongeza uwajibikaji katika taasisi” aliongezea Bw. Malya.

Mkuu wa Kitengo cha Habari TRC Bi. Jamila Mbarouk alisema kuwa kupitia tuzo hiyo TRC imezidi kupata nguvu mpya na faraja ya kufanya vyema zaidi katika kuhabarisha umma kwa njia ya mtandao kupitia kitengo cha habari cha shirika. “TRC tumeweza kujikita katika upashaji wa habari na tunatumia kujitangaza katika njia mbalimbali za mtandao” alisema Bi. Jamila.

Bi. Jamila ametoa shukurani za dhati kwa Mkurugenzi Mkuu, menejimenti na wafanyakazi wote wa TRC kwa kutoa ushirikiano mzuri kwa kitengo cha habari na kukipa nguvu za kuweza kufanya kazi kwa ufanisi, pia alitoa shukurani kwa timu ya kitengo cha habari kwa kujitoa katika kazi pamoja na ubunifu ambao umeleta heshima kubwa TRC.