Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

SERIKALI YAZIDI KUTOA HAMASA YA KULETA MAENDELEO YA NCHI KWA WANANCHI MKOANI MOROGORO


news title here
07
February
2021

Serikali inazidi kutoa hamasa ya kuleta maendeleo ya nchi kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro baada ya kuendeleza zoezi la ulipaji wa fidia katika maeneo mbalimbali yaliyobaki ambapo zoezi hilo linafanywa na Shirika la Reli Tanzania ili kupisha ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Dar es Salaam- Morogoro, Februari 2021 hivi karibuni.

Maeneo hayo ni pamoja na maeneo ya kifusi , maeneo yaliyo pitiwa na umeme,maeneo yaliyo ongezeka pamoja na wananchi ambao hawakuwepo wakati wa ufanyaji wa uthamini wa maeneo.

Wananchi mkoani humo wamehamasika katika kufanya maendeleo mbalimbali yatakayoleta faida na mapato ya nchi baada ya kupokea hundi zao.

Licha ya mikakati hiyo ya maendeleo wamefurahishwa sana na zoezi hilo na kuishukuru serikali kutekeleza ahadi ya malipo na kutenda haki kwa wananchi.

Afisa wa masuala ya jamii kutoka TRC Bi. Lightness Mngulu amesema kuwa zoezi linaendelea bila malalamiko ya aina yeyote kutoka kwa wananchi.

“Hadi sasa hatujapata malalamiko ya aina yeyote na endapo likijitokeza tunawapa taratibu za kufuata ili kukamilisha zoezi “ alisema Bi. Lightness.

Wananchi hao wanaokabidhiwa hundi wametoka katika maeneo mbalimbali ya vijijini ikiwemo kijiji cha Mikese, Tanki la maji , Kinonko , Mkambarani , Mtego wa simba , Pangawe pamoja na mtaa wa Yespa.