Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

RAIS WA MALAWI AIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA UJENZI WA RELI YA KISASA – SGR


news title here
08
October
2020

Rais wa Jamhuri ya Malawi Mhe. Lazarus Chakwera atembelea mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR kipande cha Dar Es Salaam – Morogoro katika eneo la Ilala jijini Dar es Salaam, ziara hiyo imefanyika tarehe 08 Oktoba, 2020.

Aidha, Rais Lazarus yupo nchini Tanzania katika ziara ya kikazi kwa siku tatu yenye lengo la kuimarisha uhusiano baina ya nchi ya Tanzania na Malawi.

Rais Chakwera akiambatana na wenyeji wake ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Prof. Paramagamba Kabudi, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Shirika la Reli Tanzania - TRC Prof. John Kondoro, Mkurugenzi Mkuu TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa na Menejimenti ya TRC alipata taarifa kuhusu maendeleo ya ujenzi wa reli ya Kisasa - SGR na kushuhudia ujenzi wa daraja lenye urefu wa KM 2.5 linalojengwa jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Rais Lazarus ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa uthubutu wa ujenzi wa miundombinu ambayo itasaidia kujenga uhusiano wa sekta ya biashara, uchumi na viwanda kati ya Malawi na Tanzania. Katika hatua nyingine Rais Lazarus ameipongeza serikali kwa kazi kubwa ya kujenga reli ya kisasa – SGR kwa kutumia fedha za ndani za kodi, huku akifananisha ukubwa wa kilomita mradi mzima ambao ni sawa nchi ya Malawi

“Hii ni moja ya maendeleo makubwa ya kuwa na uwezo wa kutumia pesa za ndani za walipa kodi kujenga miundombinu ambayo sio faida kwa Taifa bali kwa Afrika nzima, urefu wa hii reli ni sawa na nchi nzima ya Malawi na kama Tanzania

wameweza kujenga reli hii hata sisi Malawi tunaweza pia’’ alisema Rais wa Malawi.

Naye, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Kamwelwe alibainisha kwa kueleza jinsi sekta ya usafirishaji wa njia ya reli nchini Tanzania utakavyoshirikiana na nchi ya Malawi pamoja na nchi za jirani za Afrika katika usafirishaji wa mizigo ambao utakuwa ni tija katika ukuaji wa uchumi barani Afrika.