Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

RAIS WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO AMPONGEZA JPM KWA UJENZI WA RELI YA KISASA - SGR.


news title here
14
June
2019

RAIS WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO AMPONGEZA JPM KWA UJENZI WA RELI YA KISASA - SGR.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Felix Tshisekedi Tshilombo atembelea mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR kipande cha Dar Es Salaam - Morogoro, ziara hiyo imefanyika June 14 2019.

Ziara hiyo iliongozwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kungu Kadosa na viongozi wa ngazi ya Kitaifa, ambapo Rais alipata fursa ya kuona hatua tofauti za ujenzi wa reli ya kisasa ukiwemo utandikaji wa reli ya kisasa - SGR unaoendelea maeneo ya Vingunguti jijini Dar Es Salaam.

Aidha, Rais Felix Tshisekedi amesema kuwa lengo la ziara nchini Tanzania ni kuthibitisha mahusiano kati ya nchi ya Kongo na Tanzania kupitia ujenzi wa miundombinu ambayo itasaidia kujenga uhusiano wa sekta ya biashara, uchumi na viwanda kati ya Kongo na Tanzania.

Hata hivyo, Rais Felix Tshisekedi alitoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa uthubutu na juhudi anazofanya hasa kwenye kuimarisha miundombinu ukiwemo ujenzi wa reli ya kisasa ambao ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa Tanzania na nchi jirani.

Mh.Rais wa Kongo ameishauri Tanzania kutunza na kudumisha miumdombinu ili kuongeza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Naye, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Kamwelwe alibainisha kwa kueleza jinsi sekta ya usafirishaji wa njia ya reli nchini Tanzania utakavyo shirikiana na nchi ya Kongo pamoja na nchi za maziwa makuu katika usafirishaji wa mizigo ambao utakuwa ni tija katika ukuaji wa uchumi barani Afrika.