Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

PROFESA MBARAWA AWATAKA WAWEKEZAJI KUWEKEZA TRC


news title here
11
February
2025

Waziri wa Uchukuzi Mhe.Profesa Makame Mbarawa, Februari 11, 2025 ameshiriki ufunguzi wa Mgahawa wa Kimataifa wa KFC uliopo stesheni ya Magufuli Jijini Dar es Salaam.

Ufunguzi wa mgahawa huo ulio chini ya Dough Works Limited (DWL), ndani ya stesheni ya Magufuli umedhamiria kuwarahisishia abiria wanaosafiri na treni za SGR upatikanaji wa huduma za chakula na vinywaji na kuepusha usumbufu wakati wa safari.

Akiongea wakati wa hafla hiyo Prof.Mbarawa, amesema kuwa serikali kupitia TRC inajivunia ujenzi wa reli ya SGR kwani umewezesha wawekezaji na wafanya biashara kuwekeza katika sekta mbalimbali na hivyo kuzidi kuongeza kipato cha nchi na wananchi kwa ujumla.

"Migahawa ya KFC ni chapa kubwa kote duniani, hivyo kuuona hapa kwenye stesheni yetu ni heshima na imeliongezea jengo letu uthamani, kwa namna hii naamini wasafiri watapata chakula chenye ubora na hadhi ya Kimataifa" amesema Mbarawa.

Aidha, Mhe. Mbarawa, ameongeza kuwa kupitia uwekezaji na biashara ndani ya Majengo ya stesheni za SGR ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma utachangia ukuaji wa sekta mbalimbali kama vile kilimo na kuongezeka kwa thamani ya mnyororo wa usambazaji bidhaa na kukuza ajira kwa vijana wa Kitanzania.

Awali Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli Tanzania (TRC) Ndugu Masanja Kungu Kadogosa, aliendelea kusisitiza wafanya biashara, Wawekezaji na Wadau mbalimbali kujitokeza na kuchangamkiab fursa zinazopatikana kama vile kwenye majengo ya stesheni na mahoteli, Magala ya kuifadhi mizigo, Usafirishaji na kilimo.

"TRC bado tunafursa nyingi za uwekezaji ,tuna majengo ,magala ya kuhifadhi mizigo na usafirishaji vyote hivyo vinahitaji wawekezaji , hatusafirishi abiria tu na mizigo pia tunasafirisha, karibuni TRC tunawahakikishia kuwapa huduma bora na kuwawezesha kufanya biashara zenu kwa mazingira bora"Amesema Ndugu Kadogosa.

Katika hatua nyingine, Bwana Vikram Desai Mkurugenzi Mtendaji wa Migahawa ya KFC Tanzania, alisema uwepo wa migahawa ya KFC Tanzania ukiwemo wa stesheni ya Magufuli, umechangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza sekta ya kilimo nchini, kuwezesha maendeleo ya jamii kukuwa kiuchumi, kutoa mafunzo kwa vijana kuhusu masuala ya ukarimu na huduma kwa wateja na kuongeza thamani ya bidhaa zinazo zalishwa na Watanzania.

"Nchi ya Tanzania imefanya jambo kubwa sana katika ujenzi wa reli ya SGR, sisi kama KFC tunajivunia kuwa sehemu ya maendeleo hayo, KFC itahakikisha inatoa fursa za ajira kwa vijana wa kitanzania, kukuza kilimo kupitia ununuzi wa bidhaa za kilimo kama vile kuku na mbogamboga na mwisho kukuza uchumi wa nchi" Amesema Bwana Vikram.

Shirika la Reli Tanzania inaendelea kuwasisitiza wawekezaji kujitokeza na kuwekeza katika maeneo na fursa mbalimbali zilizopo ili kuendelea kukuza uchumi wa nchi.