Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

NAIBU WAZIRI MHE. ATASHASTA NDITIYE AFUNGUA BARAZA JIPYA LA WAFANYAKAZI LA SHIRIKA LA RELI TANZANIA - TRC


news title here
17
April
2019


Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe, Mhandisi Atashasta Nditiye afungua rasmi Baraza jipya la wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania - TRC katika ukumbi wa Bandari jijini Dar es Salaam hivi karibuni Aprili 2019.

Hafla hiyo ya ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi TRC kwa mara ya kwanza tangu kuunganishwa kwa iliyokuwa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL na Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli – RAHCO na kuanzishwa TRC.

Baraza jipya la wafanyakazi lina jukumu la kusimamia na kutetea maslahi ya wafanyakazi kupitia wawakilishi kutoka idara na vitengo vya taasisi pamoja na wajumbe wa kamati tendaji wanaotokana na wajumbe wa baraza.

Kulingana na katiba ya baraza na taratibu za kisheria Baraza lina kazi ya kupitia na kutoa maoni na kuboresha utendaji wa Shirika, pia baraza ni chombo cha kuleta upendo na umoja baina ya wafanyakazi.

Mgeni rasmi wa ufunguzi wa Baraza hilo naibu waziri Mhe. Atashasta Nditiye amelipongeza Shirika la Reli Tanzania kwa kufanya uamuzi huo wa kuundwa Baraza jipya na kuwataka wajumbe kulifanya Baraza kama sehemu wa kuwawakilisha wafanyakazi kwa lengo la kutatua matatizo changamoto na kuleta tija katika Shirika.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania - TRC alisema kuwa serikali inafuatilia Mali za Shirika ambazo zinamilikiwa na watu binafsi wamejibinafisha kwa njia zisizo halali na kuomba wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania kushirikiana katika kutoa taarifa sahihi ili rasilimali hizo zirudi kuongeza mapato kusaidia kuendesha Shirika ikiwemo kuinua maslahi ya wafanyakazi.