Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

MRADI WA UJENZI WA RELI YA KISASA KUPANDISHA THAMANI YA ARDHI


news title here
19
May
2019

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Wiliam Lukuvi afanya ziara katika Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa Soga Kibaha mkoani Pwani hivi karibuni Mwezi 2019.

Lengo ni kuona namna ambavyo wizara ya ardhi inaweza kupanga miji katika maeneo ambayo reli ya kisasa inapita, Mei 18, 2019.

Waziri Lukuvi akiambatana na Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mbunge wa Kibaha Vijijini na Maafisa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha walipata fursa ya kuzungumza na wananchi wa Vijiji vya Kwala na Soga na kuwatangazia rasmi mpango wa serikali wa kupandisha thamani katika maeneo yote ambayo reli ya kisasa inajengwa.

Katika ziara hiyo Waziri Lukuvi amewasisitiza wananchi kuacha kuuza kiholela ardhi wanazomiliki na kusubiri mpango maalum wa serikali kupanga matumizi ya ardhi katika maeneo yote ambayo Mradi wa SGR unapita ili waweze kumilikishwa ardhi na kupewa hati ili waweze kufanya shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo muhimu kiuchumi hususani eneo la Kwala ambalo Karakana na kituo kikubwa cha treni za kisasa za mizigo kinajengwa sambamba na bandari kavu itakayokuwa ikitoa huduma pamoja na reli ya kisasa – SGR na reli ya zamani – MGR.

.