Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AZINDUA RASMI KAMPENI YA UELEWA KUEPUSHA AJALI KATIKA RELI MKOANI KILIMANJARO


news title here
08
August
2020

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Dkt. Anna Mgwhira amefungua rasmi kampeni ya uelewa kwa wananchi ili kuepusha ajali katika miundombinu ya reli mkoani Kilimanjaro hivi karibuni Agosti 2020.

Mkuu wa mkoa amefungua ziara hiyo ambayo inafanyika katika mikoa ya Arusha, Tanga na Moshi ikiwa na lengo la kutoa elimu ya uelewa kuhusu matumizi sahihi ya alama za usalama katika miundombinu ya reli ili kuepusha ajali na uharibifu wa miundombinu ya reli unaoweza kutokea kutokana na kutokuwepo na uelewa wa masuala hayo.

Shirika linaendesha Kampeni ya uelewa itakayodumu kwa muda wa majuma mawili kuanzia Agosti 3 ambao wanachi watapata fursa ya kuelewa masuala mbalimbali yahusuyo usalama wa reli kupitia vyombo vya habari na mikutano ya ana kwa ana katika maeneo ya wazi na mashuleni ambapo baada ya ufunguzi huo timu ya mawasiliano imefanikiwa kufanya mkutano na wananchi katika mtaa Boma Mbuzi na kutoa elimu ya usalama wa reli katika shule ya Msingi Azimio mkoani Kilimanjaro.

Aidha Mkuu wa Mkoa ametoa pongezi zake kwa Chama Cha Mapinduzi kwa kurejesha safari za treni kanda ya Kaskazini kwani zimesadidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha shughuli za wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro

“Nipongeze Chama Cha Mapinduzi ambacho kinaongoza hivi sasa kwa kazi nzuri inayofanya kwa kurejesha usafiri wa treni ambao unatusaidia kurashisisha shughuli zetu mbalimbali za kibiashara na mahusiano ya kijamii” alisema Mkuu wa Mkoa

Pia Mkuu wa Mkoa aliwasisitiza wananchi mkoani humo kuacha shughuli za kibinadamu katika maeneo ya reli kwa kuwa hivi karibuni Shirika linatarajia kurejesha huduma za usafiri wa treni kutoka Dar es Salaam na Tanga kuelekea Moshi na Arusha hivyo hifadhi ya reli katika maeneo hayo si salama tena hivyo ni busara wananchi kuanza kuacha wazi maeneo ya reli ili treni ziweze kuhudumia wananchi kwa usalama.

“Njia yetu hii ya reli imetengewa Mita 60 za hifadhi, Mita 30 upande wa kushoto na Mita 30 upande wa kulia kama ambavyo tunafanya katika barabara, wakati ule ambao reli ilikuwa haifanyi kazi watu walilima kwenye maeneo ya reli lakini hivi sasa si salama tena kwahiyo sisi sote ambao tulikuwa tunafanya shughuli zetu kandokando ya reli inatubidi tusogeze shughuli zetu nje ya eneo la reli” alisema Mkuu wa Mkoa

Halikadhalika Mkuu wa Mkoa amelitaka Shirika la Reli Tanzania kuhakikisa linatimiza makubaliano yote yanayofikiwa kati ya Shirika, uongozi pamoja na wananchi ikiwemo kuhakikisha zinawekwa alama za usalama katika maeneo ya reli, kuweka vivuko vya kutosha, kuhakikisha maeneo ya reli ambayo wananchi watapisha yanakuwa safi lakini kubwa Zaidi ni kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wakutosha kuhusu ulinzi na usalama wa reli.