Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

WAZIRI MBARAWA AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI WA SHIRIKA LA RELI TANZANIA


news title here
14
June
2018

Waziri wa ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa leo Juni 11, 2018 amezindu rasmi bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Reli Tanzania. Hatua hiyo imefikiwa baada ya Shirika la Reli Tanzania kutokuwa na bodi kwa kipindi cha muda mrefu kufuatia kuundwa upya kwa Shirika hilo lililotokana na kufutwa kwa Kampuni mbili za RAHCO na TRL. Muungano wa Makampuni hayo mawili umefikia ili kuongeza tija kwenye utoaji wa huduma za usafiri wa reli nchini Tanzania.

Waziri Prof. Mbarawa mbali na kutangaza rasmi bodi mpya, pia alipata fursa ya kutoa vyeti kwa wajumbe wa bodi ya iliyokuwa TRL na RAHCO ambayo imemaliza muda wake. Bodi mpya ikiongozwa na Mwenyekiti wake Prof. John Kondoro pamoja na katibu wake Bwana. Masanja Kadogosa inajumuisha wajumbe saba ambao ni Bw. Edson Mweyunge-Mjumbe, Bi. Wolgang Ephraim Salia, Bi. Rukia Diwani Shamte, Dkt. Jabir Kawe Bakari, Eng. Karim Mataka, Bw. Mohammed Mashaka Mabuyu na Bw, Mativila.

Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wa bodi umefanyika Kwa mujibu wa sheria ya Reli, Bodi ya Wakurugenzi inaundwa na Mwenyekiti ambaye atateuliwa na Rais ambaye ana uelewa wa masuala ya reli, wajumbe saba watakaoteuliwa na Waziri ambao wana utaalamu wa masuala ya Uhandisi, biashara, uchumi, sheria na masuala ya utumishi. Bodi hii, imezingatia matakwa ya kisheria na sasa kama muonavyo, wajumbe wa Bodi hii wametoka katika taasisi zenye ujuzi na utalaam wa maeneo haya. Aidha, wamebobea hasa katika taaluma zao ambazo ni muhimu katika kusimamia sekta hii muhimu.

Aidha mbali na kutangaza rasmi bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Reli, Waziri Mbarawa ameiagiza bodi hiyo kuanza kazi mara baada ya uzinduzi huo na kuitaka ihakikishe kuwa wanaajiriwa wataalam wanaokwenda na kasi ya teknolojia, usimamia mradi wa reli ya kisasa (SGR) unafanyika kwa Saa 24, kuharakisha zabuni ya kupata mabehewa na vichwa vitakavyotumika kwenye mradi wa reli kisasa (SGR) pindi utakapokamilika na Kujenga vidhibiti mwendo kwenye makutano ya reli na barabara ili kuzuia ajali.