Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

KAMATI ZA BUNGE ZAIPONGEZA TRC, ZATOA MAELEKEZO


news title here
09
November
2024


Kamati ya Bunge ya Bajeti na Kamati ya Bunge ya Miundombinu zimeshiriki Semina ya Wabunge kuhusu utendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa

Stesheni ya SGR ya John Pombe Magufuli jijini Dar es Salaam, Novemba 09, 2024.

Lengo la Semina hiyo ni kuwajengea uwezo wabunge ili wafahamu vyema shuhguli za uendeshaji wa SGR na hali ya miundombinu katika uendeshaji wa treni za mwendokasi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Moshi Kakoso ameipongeza Serikali kwa kulijenga Shirika na kulifanya kuwa la Kimataifa.

"TRC mmefanya kazi na jitihada kubwa sana na kulifanya Shirika letu kuzungumziwa na nchi mbalimbali, tumeshuhudia viongozi wa nchi za SADC na Afrika Mashariki wametembelea kuona mambo makubwa yaliofanyika" amesema Mhe. Kakoso.

Aidha, Mhe. Kakoso amewataka Wabunge kuendelea kuhimiza Serikali kufanya jitahada za kuikamilisha mradi wa SGR ili uweze kuunganisha nchi na maeneo mbalimbali ya nchi na nchi jirani.

"Nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge, tungekuwa hatuna dhati tungeweza kuliangusha Shirika lakini hoja zetu na michango yetu imeleta tija katika maendeleo haya, naomba tuendelee kupambana reli hii ikamilike " Amesema Mhe. Kakoso.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti Mhe. Oran Njeza amesema kuwa Tanzania imewakomboa nchi nyingi kisiasa sasa ni muda wa kuzikomboa nchi hizo kiuchumi kwa kuunganisha huduma za reli ili kurahisisha uvushwaji wa uchumi baina ya nchi hizo zote kwa maslahi mapana na kuinua uchumi wa Taifa.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli Tanzania Bi. Amina Lumuli amesema kuwa elimu na mafunzo kupitia semina ya wabunge itawawezesha kufahamu vyema dira ya Shirika ambayo imejikita katika kutoa huduma bora ndani na nje ya nchi.

TRC imeendelea kutoa huduma bora katika uendeshaji wa SGR ambapo ndani ya kipindi cha miezi minne ya uendeshaji imeweza kusafirisha zaidi ya abiria 800,000.

"Kupitia semina hii ,Wabunge watafahamu vyema dira ya Shirika ambayo imejikita katika kutoa huduma bora ndani na nje ya nchi, utoaji wa huduma ni endelevu na hata kwenye uendeshaji wa SGR tumekuwa na mafanikio makubwa" Amesema Bi. Amina

Bi. Amina ameongeza kuwa Shirika la Reli Tanzania linaongozwa na mpango mkakati ambao unaliwezesha Shirika kutekeleza majukumu yake ya kila siku katika kuwahudumia wananchi na kuchangia pato la Taifa.

Kamati za Bunge zimekuwa zikifanya ziara Mara kwa Mara kutembelea miradi ya TRC ili kuhakikisha ufanisi na ubora katika utekelezaji