Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

KAMATI YA BUNGE PIC, WANANCHI ACHENI KUHUJUMU MIUNDOMBINU SGR


news title here
14
November
2024

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji ya Mitaji ya Umma - PIC imefanya semina na Viongozi wa Shirika la Reli Tanzania - TRC kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la stesheni ya SGR la John Pombe Magufuli jijini Dar es Salaam Novemba 14,2024.

Lengo la semina ya PIC ni kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi na uendeshaji kwa ujumla, tangu safari za SGR zilipoanza usafirishaji wa abiria Dar es salaam hadi Morogoro mapema mwezi Juni 2024, hadi kufikia Dodoma mwezi Agosti 2024 zilipozinduliwa rasmi na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.

Mwenyekiti wa PIC Mhe. Augustine Vuma ameipongeza serikali ya awamu sita kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa SGR ambao ni faida kwa nchi ya Tanzania na Afrika Mashariki na kati kwa ujumla.

"Zaidi ya Dora za kimarekani bilioni 10 zimewekezwa katika kufanikisha mradi wa SGR " ameeleza Mhe. Vuma

Akizungumza na wanahabari, Mwenyekiti wa PIC Augustine Vuma amesema kuwa kupitia mradi wa SGR hadi sasa faida ya Bilioni 20 zimepatikana katika usafirishaji wa abiria kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro na Dodoma na kuongeza pato kubwa kwa shirika na taifa.

" Hii ni reli Mseto kwa maana inasafirisha abiria na mizigo, ifikapo mwakani 2025 usafirishaji wa mizigo rasmi utaanza na kuleta faida kubwa sana " alisema Augustine Vuma

Naye Naibu Waziri kutoka Wizara ya Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ametaja changamoto kadhaa ambazo zinarudisha nyuma na kukwamisha maendeleo ya mradi wa SGR hasa kwa vipande vilivyokamilika ikiwemo watu kuhujumu miundombinu ya reli kwa kukata nyaya za umeme, kuharibu fensi, na kusababisha uharibu wa miundombinu ya reli na hasara.

"Tumetoa maelekezo na ushauri kwa vipande ambavyo havijakamilika ujenzi pia tumepokea mipango na mikakati ya maendeleo kutoka TRC " amesema Mhe. David Kihenzile

Serikali itaendelea kuwa bega kwa bega na shirika la reli Tanzania-TRC katika kuhakikisha inatekeleza vyema miradi ya kimkakati ikiwemo mradi wa ujenzi wa SGR ili kuweza kuinua uchumi wa nchi na kuongeza pato la taifa kupitia Wizara ya Uchukuzi.