Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

JESHI LA POLISI KIKOSI CHA RELI WAFANYA MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA


news title here
10
December
2019

Makao makuu ya polisi kikosi cha reli wamefanya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto hivi karibuni , maadhimisho hayo yanayofanyika kila mwishoni mwa mwaka kuanzia Tarehe 25 Novemba hadi 10 Disemba .

Afisa Mfawidhi kwenye Makao ya Taifa ya Watoto Kurasini Bi. Beatrice Lawrence amesema kuwa tatizo la unyanyasaji hasa kwa watoto wa jinsia zote limekua likiongezeka sana katika jamii hivyo kupitia maadhimisho haya jamii itambue haki za watoto na kuacha kuwafanyia watoto vitendo vya kikatili .

“ Wazazi wawe makini sana sababu matatizo haya yanaanza kwa watu wakaribu wanaowazunguka , alisema Bi. Beatrice “.

Bi. Beatrice aliiasa jamii kuwa Karibu katika kuwalinda watoto na si kuwafanyia vitendo viovu hali ambayo itavuruga malengo na saikolojia ya watoto na kushindwa kupata haki zao za msingi ikiwemo malazi , mavazi na elimu iliyo bora .

“ vitendo vya kikatili vipo vingi na havitokei kwa watoto yatima tuu hata wazazi wanaweza wafanyia watoto wao , hivyo hatuna budi kuwalinda watoto, aliongezea Bi. Beatrice “.

Hata hivyo Bi. Beatrice ametoa Shukrani za dhati kwa Makao Makuu ya Polisi Reli kwa kutoa muda wao kuja kuwaona watoto hawa wenye uhitaji na kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vifaa vya kufanyia usafi pamoja na vifaa vya kusomea .

Naye SP Zabron Ibeganisa kutoka kikosi cha polisi reli amesema kuwa kikosi cha polisi kimejipanga vyema katika kutokomeza tatizo la unyanyasi wa kijinsia kwani limekua kubwa kuanzia kwenye malezi na watu wenye tabia za uovu .

“ Tunahakikisha kuwa tunamshughulikia mtu yeyeto anayejihusisha na unyanyasi wa kijinsia na kumchukulia hatua kali za kisheria , alisema SP Ibeganisa “.

Pia SP Ibeganisa amewataka watu wanaofika kituoni na kutoa ripoti ama kuwakabidhi watoto walionyanyaswa kijinsia wawe wawazi na kutoa ripoti kamili ili kuweza kuchukua hatua za haraka kwa wahusika hao .

Mwenyekiti wa Kitengo cha Dawati la jinsia na watoto kutoka katika kituo cha polisi reli Emelda Mwakilembe amesema kuwa jamii izidi kupatiwa elimu ya kutosha kuhusu kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia na ihamasike kuwatunza watoto kwani watoto ndio taifa la kesho litakalo ijenga nchi .

“ Tunapata kesi nyingi na watoto kufikia kutoka makwao na kudandia treni hasa katika mikoa ya kanda ya ziwa ikwemo mkoa wa Kigoma , Mwanza na Tabora, alisema Afande Mwakilembe”.