Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​CHAMA CHA SAIDIA WAZEE TANZANIA (SAWATA) WATEMBELEA MRADI WA SGR.


news title here
10
August
2020

Chama cha saidia Wazee Tanzania watembelea mradi wa wa ujenzi wa reli ya kisasa -SGR kwa kipande cha kwanza Dar mpaka Ruvu mkoa wa pwani hivi karibuni Agosti 2020.

Chama hiki kinaundwa na wazee wastaafu wa kada mbali mbali wengi wao ni wastaafu wa jeshi na walimu, kimeundwa chama hiki kwa lengo la kuwakwamua kimaisha wazee mara baada ya kustaafu .

Chama hiki kinatekeleza majukum yake katika jiji la Daresalaam maeneo ya Uwanja wa Mkapa, Temeke.

Wazee hawa wana utaratibu wa kutembelea Miradi tofauti tofauti haswa ya kimkakati ukiwemo huu wa standard Gauge – SGR na wamefurahishwa sana na kutoa shukurani za dhati mara baada ya kupanda treni ya Mkandarasi na kutembea nayo kutoka ruvu hadi Soga na kusema wameyaonja Matunda ya Uhuru,

Aidha wametoa shukurani za dhati kwa Rais wa Awamu ya tano Dokta John Josseph Pombe Magufuli pamoja na shirika la Reli Tanzania TRC haswa kwa kuwapa fursa hii ya kuweza kutembelea mradi huu wa kipekee wa SGR kama kundi la Wazee wa kwanza kutembelea mradi huu.