Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

BENKI YA DUNIA YARIDHISHWA NA KASI YA UKARABATI WA RELI YA KATI DAR – ISAKA


news title here
09
March
2020

Wafadhili wa ukarabati wa reli ya kati Benki ya Dunia wameridhishwa na ukarabati wa reli ya kati – TIRP katika ziara waliyoifanya kuanzia Dar es Salaam hadi Tabora - Isaka, hivi karibuni Machi, 2020.
Lengo ni kujua kiwango na ubora wa nyenzo zinazotumika katika ukamilishaji wa ukarabati huo, ziara hiyo iliyofanywa katika njia nzima ya reli ya kati ambapo maafisa kutoka benki ya Dunia wakishirikiana na wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania - TRC pamoja na wahandisi washauri kuoka DOHWA na wakandarasi kutoka China ambapo walipata fursa ya kukagua ujenzi wa madaraja, utanduaji wa reli ya zamani na kuweka reli mpya pamoja na kutembelea katika stesheni tofauti.
Mhandisi kutoka Benki ya Dunia Allen David Natai amesema kuwa wamefurahishwa sana na maendeleo ya ukarabati wa reli ya kati kwa sababu aslimia kubwa ya ukarabati huo upo ukingoni kukamilika halikadhalika ujenzi wa madaraja umeshakamilika na kubaki baadhi ya sehemu chache.
“Kiukweli reli ilipotoka na ilivyo hivi sasa ni jambo la kushukuru, kwani njia ya reli ilikuwa katika hali mbaya ila kwa kupitia ukarabati huu tumeona njia imenyooka vizuri na hata tukiwa njiani treni haiyumbi” alisema Mhandisi Natai.
Hata hivyo wafadhili hao walipata nafasi ya kufanya mikutano katika sehemu mbalimbali za kambi ya ujenzi wa reli hiyo kwa lengo la kujadili hatua za ukarabati ulipofikia pamoja na kujua mikakati ya wakandarasi katika kuhakikisha ukarabati unakamilika kwa wakati kulingana na mkataba wa ujenzi huo. Msimamizi wa masuala ya kijamii Bi. Catherine Mroso amesema kuwa ukarabati huo wa mradi umeweza kuifikia jamii kwa kiasi kikubwa sana na mpaka sasa vijana takribani 2,000 wameweza kupata ajira katika maeneo mbalimbali ya mradi.
“Sisi kama kitengo cha jamii cha shirika tunahakikisha kwamba jamii inashiriki katika miradi ya reli pamoja na kuhamasisha jamii mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kujiepusha na magonjwa yanayotoka pia na muingiliano wa watu kama Ukimwi” alisema Catherine.
Naye Mkurugenzi msaidizi ufuatiliaji miradi sekta ya uchukuzi Bw. Meena Aunyisa amesema kua ni hatua nzuri ya ukarabati huo ambayo serikali ya awamu ya tano imechukua kwani njia ya reli ni ya urahisi na nafuu kwa wananchi wengi nchini na usafirishaji ukiboreshwa hata mzunguko wa mara kwa mara wa kibiashara sehemu mbalimbali za mikioa itakua na unafuu.