Treni za Masafa Marefu
Kusafiri na Watoto
Chini ya Miaka 6: BURE
Kuanzia miaka 7 hadi miaka 13:
- Daraja la Pili Kulala: Nusu ya bei ya Tiketi ya mtu mzima
- Daraja la Pili Kukaa: Nusu ya bei ya Tiketi ya mtu mzima
- Daraja la Tatu: Nusu ya bei ya Tiketi ya mtu mzima
Zaidi ya miaka 14:
- Daraja la Pili Kukaa: Bei ya mtu mzima
- Daraja la Pili Kulala: Bei ya mtu mzima
- Daraja la Tatu: Bei ya mtu mzima
Kukata Tiketi
- Unapotaka kukata tiketi fika na kitambulisho kimoja kati ya hivi; Cha kupigia kura, Cha uraia, Leseni ya Udereva, Kitambulisho cha kazi, Kadi ya bima ya afya, na barua ya utambulisho kutoka Serikali ya mtaa unaoishi.
- Abiria anaweza kubadili siku ya safari masaa matatu kabla ya treni kuanza safari.
- Tiketi za kundi zinakatwa kwa watu wasiopungua saba. Ambao wanaweza kukatiwa tiketi ya pamoja au kila mmoja akakatiwa tiketi yake.
- Abiria anaweza kukata tiketi mwezi mmoja kabla ya safari kwa Daraja la Kwanza na la pili, kwa daraja la tatu abiria anaweza kukata tiketi siku nne(4) kabla ya safari.
Vifurushi
- Daraja la Pili Kulala: Kilogramu 40.
- Daraja la Pili Kukaa: Kilogramu 30.
- Daraja la Tatu: Kilogramu 20.