Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​ZOEZI LA UTWAAJI ARDHI MRADI WA SGR TABORA–KIGOMA LAENDELEA KWA KASI


news title here
19
September
2026

Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaendelea na zoezi la utwaaji wa ardhi linaloambatana na uhamishaji wa makaburi katika Kipande cha Sita cha mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Tabora hadi Kigoma linaloendelea kufanyika wilaya ya Uvinza, mkoani Kigoma.

Zoezi hilo linalenga kupisha maeneo mbalimbali ya ujenzi wa mradi huo wa kimkakati ili ikiwemo ujenzi wa njia kuu ya reli, madaraja na vivuko.

Mthamini kutoka TRC, Bw. Hassan Mbaga, ameeleza kuwa zoezi hilo la uhamishaji makaburi linagusa vijiji mbalimbali vikiwemo Nyangabo, Nguruka, Gweru, Malagarasi, Mpeta, vilivyopo katika wilaya ya Uvinza - Kigoma.

Katika kusaidia mchakato wa zoezi hilo, Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, Bw. Hussein Katelanya , amebainisha kuwa zoezi la uhamishaji makaburi linafanyika kwa ushirikiano wa karibu kati ya TRC, Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya, na Timu ya Huduma za Afya Kinga.

Hata hivyo Bw. Katelanya ameeleza kuwa usalama wa afya umepewa kipaumbele cha juu kwa kuhakikisha waandaji na wachimbaji wanatumia vifaa kinga (PPE) kikamilifu pamoja na hatua za usafi zinaratibiwa kwa kutumia maji tiririka, sabuni, na dawa kwa ajili ya kutibu miili na kutakasa maeneo husika pamoja na washiriki wa zoezi hilo.

Mbali na vipengele vya kiafya na mazingira, staha na heshima kubwa vimezingatiwa wakati wote wa kuhamisha miili ya marehemu kutoka kaburi moja kwenda jingine wakishirikiana na ndugu wa marehemu kikamilifu katika kila hatua ya mchakato huo ili kuhakikisha taratibu zote za kifamilia na kijamii zinazingatiwa,

Viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali.