Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

TRC NA WCF ZASAINI MAKUBALIANO YA UWEKEZAJI WA Bil. 65*


news title here
02
October
2026

Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF), zimetia saini hati ya Makubaliano ya Ujenzi wa Ukumbi wa Mikutano katika hafla iliofanyika ukumbi wa Mikutano Stesheni ya SGR Jakaya Kikwete Morogoro Oktoba 2, 2026.

Katika Makubaliano hayo patajengwa kumbi za Mikutano ishirini na Sita ( 26) zenye kukidhi Idadi ya watu kuanzia watu 10 mpaka 600 kulingana na mahitaji na pia hoteli ya nyota nne yenye vyumba takribani tisini na moja katika eneo la stesheni ya SGR Jakaya Mrisho Kikwete.

Ujenzi huo unakadiriwa kugharimu shilingi za Kitanzania Bilioni 65.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji Saini Makubaliano hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe.Deus Sangu, ameeleza azma ya serikali ya awamu ya sita kushirikisha sekta mbalimbali za kiserikali kukuza uchumi wa nchi na kuongeza Ajira Kwa vijana.

Aidha, Mhe. Sangu, amezitaka sekta zingine za serikali na binafsi ziige mfano wa TRC na WCF wa kushirikiana pamoja kuendeleza vitega uchumi ili kutimiza lengo kuu la serikali la utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Nchi kuelekea 2050.

Nae Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe.David Kihenzile, amesema kuwa uendelezaji wa miundombinu ya reli nchini utaendelea kuleta mabadiliko katika maeneo mbalimbali ya nchi na kufungua fursa za kiuchumi na kuwataka Watanzania kuchangamkia fursa zinazojitokeza.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kihenzile, amesema kuwa licha ya Serikali kujenga reli kusafirisha mizigo na abiria, itajikita kuhakikisha TRC inatumia rasilimali ilizonazo Kwa kushirikiana na mashirika mengine kufungua fursa za Uwekezaji ikiwemo ujenzi wa majengo ya biashara, kwenye kilimo, utalii, viwanda nakadhalika.

Awali Mhe. Kihenzile, aliendelea kuialika sekta binafsi kuwekeza katika sekta ndogo ya reli, kufuatia fursa iliyoletwa na mabadiliko ya Sheria ya reli na 10 ya mwaka 2017 iliofanyiwa maboresho mwaka 2023 ma kusainiwa na Rais wa Tanzania, ikiwa ni jitihada za kuruhusu Uwekezaji katika maeneo ya reli ili kuendeleza sekta ya reli na kujenga uchumi imara wa nchi kuelekea dira ya maendeleo ya nchi 2050, ambaypp sekta binafsi imepewa 70% ya utekelezaji wake.

Wakati juo huo, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi TRC Bw.Jaffer Machano, amesema ujenzi wa kumbi za Mikutano na hoteli ya nyota nne utakaofanywa na WCF umekuja wakati sahihi ikizingatia kuwa Kwa siku TRC inasafirisha abiria zaidi ya 2800 kati ya Dar es salaam na Morogoro.