Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

JESHI LA POLISI KIKOSI CHA RELI TANZANIA LAFANYA DORIA, WATUHUMIWA 7 WAKAMATWA


news title here
18
December
2020

Jeshi la polisi kikosi cha reli Tanzania lafanya doria na misako mbalimbali katika Mikoa ya Dar es Salaam, Dododma, Morogoro na Pwani na kukamata watuhumiwa saba (7) wakituhumiwa kwa makosa ya wizi wa mali za Shirika la Reli Tanzania – TRC, na mali za mkandarasi wa mradi wa ujenzi reli ya kisasa - SGR YAPI MARKEZI, taarifa imetolewa wakati wa mkutano na wandishi wa habari makao makuu ya jeshi la polisi kikosi cha reli Tanzania jijini Dar es Salaam mapema Disemba 18, 2020.

Kamanda wa polisi kikosi cha reli kanda ya Dar es Salaam Sebatian Mbuta amebainisha kuwa jeshi la polisi lilifanya dolia na misako mbalimbali kuanzia Disemba, 05 mpaka Disemba 17, 2020. Katika Mkoa wa Dar es Salaam, Dodoma katika Wilaya ya Bahi kijiji cha Chifutuka, Morogoro katika Wilaya ya Kilosa kijiji cha Kimambila na Mkoani Pwani Wilaya ya Kibaha katika kijiji cha Mwmbeni, Kongowe.

Katika hatua nyingine Kamanda wa polisi kikosi cha reli, aliweka bayana mali zilizokamatwa ambazo ni jumla ya lita 1663 za mafuta aina ya dizeli, chuma cha treni “Cylinder break”, Viunganishi vya treni vinavyoitwa TM Lugs, Mashine ya kuvuta maji, tenki la kuhifadhi maji na mafuta pamoja na mabomba aina ya PVC 29.

Aidha, Kamanda Mbuta ameeleza kuwa upelelezi wa majalada yote umekwisha kukamilika na taratibu za haraka za kuwafikisha watuhumiwa mahakama unafanyika, hata hivyo Kamanda ametoa wito kwa wananchi wote kuwa jeshi la polisi kikosi cha reli linaendelea na zoezi la ulinzi wa miundombinu ya reli na litawachukulia hatua kali za kisheria kwa yeyote atakae kamatwa na kosa la uhujumu wa miundombinu ya reli.

“Napenda kutoa wito kwa wananchi wote kwamba jeshi la polisi kikosi cha reli Tanzania tukoimara tunaendelea na doria pamoja na misako katika maeneo ambayo miundombinu ya reli imepita, napenda kuwatahadharisha wananchi wawe walinzi wa miundombinu ya reli, vile vile natoa onyo kali kwa yeyote atayetaka kuhujumu miundombinu ya reli tutamkama na hatua kali za kisheria zitachukuliwa” Kamanda Mbuta alisema.